Daktari bingwa wa tiba ya uzuwiaji wa magonjwa James Hamblin alifanya utafiti kuhusu utakatishaji wa ngozi ambao hivi karibuni umechapishwa katika kitabu.
“Ninajihisi vizuri kabisa ,”alijibu dokta James Hamblin alipoulizwa anajihisi vipi baada ya kuishi bila kuoga kwa kipindi cha miaka mitano.
” Unazowea tu”, ameiambia BBC akiwa nchini Marekani.
Hamblin ana umri wa miaka 37, na ni mtaalamu aliyesomea taaluma yake katika Chu kikuu cha Yale University kitengo cha huduma ya afya ya umma na ni daktari bingwa wa tiba ya kuzuia magonjwa.
Hamblin hatahivyo anasisitizia juu ya umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni lakini anasema sio lazima kuosha sehemu nyingine za mwili mara kwa mara
Hamblin hatahivyo anasisitizia juu ya umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni lakini anasema sio lazima kuosha sehemu nyingine za mwili mara kwa mara
Ni mmoja wa waandishi wa jarida la Marekani -The Atlantic , ambamo aliandika taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari kinachosema :Niliacha kuoga , na maisha yangu yameendelea vyema.
“Tunatumia miaka muda wa miaka miwili maishani mwetu kwa kuoga tu. Muda huo unaweza kuzalisha kiasi gani cha pesa na maji na pesa tunavyotumia katika kuoga si vinapotea bure?” anasema katika taarifa yake katika katika jarida hilo la mwaka 2016.
Mwaka huu alichapisha taarifa nyingine yenye kicha cha havbari kinachosema : Unaoga kupita kiasi.
Hata hivyo anasisitiza kuwa watu wasiache kunawa mikono kwa sabuni, Dkt James anaamini kuwa hatupaswi kuoga sehemu nyingine za mwili mara kwa mara.
Tunapoacha kuoga mara kwa mara tunapata vimelea, lakini sio wote wanaoweza utusababishia matatizo
Tunapoacha kuoga mara kwa mara tunapata vimelea, lakini sio wote wanaoweza utusababishia matatizo
Aliacha kuoga kama jaribio
Kwahiyo alipoulizwa ni kwanini aliacha kuoga , alitulia kisha akafikiria na kujibu:
“Kusema kweli ni hadithi ndefu kwakweli inahitaji kuandika kitabu kuelezea ni kwanini. Lakini nilitaka kujua ni nini kinachoendelea .”
“Ninafahamu watu wengi ambao wanaoga mara chache sana. Nilifahamu kuwa inawezekana , lakini nilitaka kujaribu ili nione kutooga kutakuwa na athari gani .”
Na mwaka 2015, alifanya uamuzi. Ni nini ulichokigundua? Na umepata athari gani?
” Baada ya kutooga muda mrefu mwili unazoea zaidi na zaidi kwahiyo haunuki vibaya usipotumia sabuni au manukato .”
“Na mwili wako haupati mafuta unapoacha kutumia sabuni kali .”
“Lakini la kubwa la kuelewa ni kwamba inachukua muda kuona athari hizi, hazijitokezi haraka, sio mara moja .”
Miili yetu ina uhusiano mkubwa na mfumo wa kinga ya mwili kwani huwa kiunganishi cha maisha ndani ya mwili na mazingira tunamoishi
Miili yetu ina uhusiano mkubwa na mfumo wa kinga ya mwili kwani huwa kiunganishi cha maisha ndani ya mwili na mazingira tunamoishi
Alisisitiza kuwa kwa upande wake mabadiliko ya kutonuka kwa mwili na kutoka jasho yalikuwa ya polepole: alianza kwa kutumia sabuni kidogo, shampuu na manukato na kuoga mara chache , na akaendelea kufanya hivyo kila siku.
” Kulikuwa na wakati ambapo nilihisi ninataka kuoga kwasababu nilihisi ninatamani kuoga na nilikuwa ninanuka vibaya. Lakini nikajitahidi kuendelea na hisia ya kutaka kuoga ikatoweka ikawa ikinijia mara chahce sana .”
Miaka minne iliyopita
Katika taarifa aliyoiandikwa mwaka 2016 , Hamblin aliandika “harufu ya mwili inatokana na bakteria wanaoishi kwenye ngozi wetu na kula mafuta yanayotolewa mwilini mwetu kwa jashokwa njia ya vinyweleo .”
Mtu anayeoga mwili
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Tunashambuliwa mara kwa mara na vimelea , lakini si wote wanaotusababishia matatizo.
Kujipaka mafuta katika mwili wetu na nywele kila siku ” huondoa aina ya uwiano baina ya mafuta na bakteria. wanaoishi ” ndani yake.
“Unapooga kwa nguvu kila wakati, unaharibu bayoanuwai. Huonezeka idadi yake haraka, lakini bayoanuwai hawa hawan uwiano na hupenda aina fulani ya vimelea ambao hutengeneza harufu ya mwili ,”alielezea katika taarifa yake.
Lakini, baada ya muda, mchakato wa udhibiti hufanyika : “bayoanuwai yako hufikia kiwango cha kuwa tabiti na huwezi kunuka vibaya tena . Hautoi harufu kama ya uwa la waridi hatahivyo…unanuka tu kama mtu wa kawaida “.
Kwa mujibu wa BBC Katika mahojiano yaliyochapishwa mwaka huu katika wavuti wa Chuo Kikuu cha Yale University , Hamblin alithibitisha kuwa sio kwamba hakunuka lakini vimelea wa mwilini mwake hawakutoa harufu zaidi kuliko ya kawaida.”