IGP Atekeleza Agizo la JPM, Awashughulikia Askari Hawa




INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro ametekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuwaondoa katika vituo vyao vya kazi, askari polisi kwa uzembe kwa kutowajibika ipasavyo hali iliyosababisha kuhujumiwa kwa miundombinu ya reli.

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime, amesema tayari viongozi hao walishaondolewa Mlandizi na nafasi zao kupangiwa wengine.

 

Kwa mujibu wa Misme, katika mabadiliko hayo, IGP Sirro aliwahamisha aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mlandizi (OCD), Mrakibu wa Polisi (SP) Severine Samwel Msonda na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mlandizi (OCS), Mrakabu Msaidizi wa Polisi (ASP) Michael Erick Kaniki, kwenda katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani.

 

Amesema Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Gairo, SP Julieth Lyimo, sasa anakuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mlandizi huku Joel Aidanus Mkuche aliyekuwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, akitumwa kuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mlandizi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mhhh. Nchi yetu inataka Jemedari kama Magu.
    kote yupo, anajua mapigo ya nchi, Bunda yupo , Songwe yupo
    Mto wa Mbu yupo, Rulenge yupo, Chalinze yupo, Kidodi yupo,
    Dosi Dosi yupo,Mpwayungu yupo, Mlanndizi yupo na Kote nchini

    Nani kaama Magufuli..!!! Baba lao.

    Sirro, Rai yangu, si kuwahamisha kituo tuu, Demot 2 Ranks na badilisha watumikie JKT miezi 24 na watumikie Magereza mwaka

    Simbachawene, Sirro tuna Imani nanyi ktk unyooshaji.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad