Jay Z am-copy Prof Jay Bongo Dar Es Salaam

 


Leo ni 'Throwback Thursday' maarufu kama TBT, watu wengi hutumia siku hii ya Alhamisi kujikumbusha kumbukumbu za matukio yao yaliyopita kwa kushea picha, video fupi au hata stori kupitia mitandao ya kijamii.

 

Kwenye muziki nataka nikurudishe nyuma kidogo ambapo mpaka mwaka 2001 ambapo msanii Prof Jay alipotoa album yake ya machozi jasho na damu na kwenye album hiyo kuna ngoma ya Bongo Dar Es Salaam aliyomshirikisha Lady Jaydee.


Ukisiliza vizuri mistari ya wimbo huo Prof Jay amezungumzia mambo yote yanayohusu Jiji la Dar Es Salaam kuanzia aina ya watu, tabia, vitu, mazingira, biashara, starehe, chuoni, daladala, mitaani na sehemu zote za Jiji kama Sinza Kinondoni na Mjini.


Pia hakuacha kutaja sifa za jinsia za watu wanaofanya matendo hayo ya kimjini mjini yaani wanaume, wanawake, watoto, wanafunzi hadi wazee, sasa huyo alikuwa ni Prof Jay ft Lady Jay Dee Bongo Dar Es Saalam.


Sasa turudi kwa Jay  Z ambapo miaka 11 iliyopita yaani 2009 aliachia kazi ya wimbo wake wa 'empire state of mind' maarufu kama New York, ambayo akimshirikisha Alicia Keys.


Jay Z yeye ameanza kwa kuisifia sehemu za Jiji hilo na mitaa yake, stori za kutisha, kazi zinazofanyika kama kuuza bangi na michezo haramu pia akasema unaweza ukaenda ukawa mtu mzuri lakini baada ya kuishi utabadilika na kuwa mtu mwenye tabia mbaya.


Ukizikiliza ngoma hizo mbili hazina tofauti kwani 'idea' zimeendana kuanzia Prof Jay alipoamua kumshirikisha Lady Jaydee halafu kule Jay Z alimshirikisha Alicia Keys, ambao wasanii hao wa kike wote wameimba viitikio.


Pia hata ukisikiliza kwa umakini beat zao zina mfanano fulani hivi kwa mbali na hata style yao ya ku-rap ilikuwa sawa, swali la kizushi je Jay Z amem-copy Prof Jay

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad