Joe Biden asema utawala wa Trump 'umeharibu' vitengo vya usalama




Vitengo muhimu vya usalama vimefanyiwa uharibifu mkubwa chini ya utawala wa rais Donald Trump , rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema.
Bwana Biden alisema kwamba timu yake haipati habari inazohitaji kutoka kwa idara ya ulinzi wakati ambapo inajiandaa kuchukua mamlaka.

Alizungumza baada ya kupatiwa habari na maafisa wa usalama pamoja na wale wa masuala ya sera za kigeni.

Bwana Biden anachukua mamlaka tarehe 20 mwezi Januari lakini rais Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Kwa wiki kadhaa baada ya uchaguzi huo wa Novemba 3 , bwana Biden alizuiliwa kupata habari muhimu za kijasusi , ikiwa ni muhimu na utaratibu wa kawaida katika mchakato wa kumkabidhi rais mteule mamalaka.

Kufuatia matamshi ya Joe Biden siku ya Jumatatu , kaimu waziri wa ulinzi Christopher Miller alisema kwamba maafisa wamekuwa wakifanya kazi kwa utaalamu mkubwa kuunga mkono mpito.

Idara ya ulinzi imewahoji watu 164 na zaidi ya maafisa 400 na kutoa nakala 5000 za stakhabadhi - zaidi ya zilizohitajika na kundi la mpito la bwana Biden, alisema.

Msemaji alisema kwamba Pentagon imekuwa wazi na kundi la bwana Biden.

Katika hotuba alioitoa katika mkutano wa video bwana Biden alisema kwamba kundi lake linakabiliwa na vizuizi katika idara ya ulinzi hususan afisi ya usimamizi na bajeti.

''Kufikia sasa , hatupati habari zote ambazo tumehitaji kutoka kwa utawala unaoondoka katika vitengo muhimu vya usalama'', alisema.

''Kwa upande wangu huo ni ukosefu wa uwajibikaji''.

Rais huyo mteule aliongezea kwamba kundi lake lilitaka kujua hali ya wanajeshi wa Marekani kote duniani na kwamba maadui wa taifa hilo huenda wakachukulia tofauti zilizopo na kusababisha mkanganyiko.

Alisema kwamba idara nyingi muhimu za kiusalama zimefanyiwa uharibifu mkubwa.

Nyingi hazina maafisa wa kutosha na motisha iko chini. Sera zilizokuwa zikitumika hazina tena thamani ama hata zimetupiliwa mbali.

Bwana Trump alimfuta kazi waziri wake wa ulinzi Mark Esper muda mfupi baada ya uchaguzi baada ya waziri huyo wa zamani kukataa kupeleka jeshi barabarani kukabiliana na waandamanaji.Hatua ya rais Trump kuwaweka watu watiifu katika idara hiyo imewatia wasiwasi wapinzani wake ambao wanachukulia kuwa jaribio la kusababisha ghasia katika wiki za mwisho za utawala wake


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad