Johnson aitisha mkutano wa dharura kuhusu marufuku ya safari za ndege

 


Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson leo ataongoza mkutano wa dharura, wakati ambapo nchi kadhaa zinaendelea kuzizuia ndege zao kwenda Uingereza ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa nchini humo. 

Johnson ameitisha mkutano wa kamati ya dharura ya mawaziri kujadili marufuku ya safari za ndege za abiria za kimataifa. 


Nchi nyingi za Ulaya tayari zimezuia ndege na wasafiri kutoka Uingereza, huku nchi zaidi zikitarajiwa kuchukua uamuzi kama huo. Shirika la Afya Duniani, WHO pia limetoa wito wa hatua kali kuchukuliwa Ulaya, ambayo hadi sasa zaidi ya watu 500,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.


 Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel jana walizungumza kwa njia ya simu kuhusu suala hilo.


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad