Jopo la Wanasayansi Duniani Laitaka Ulaya iungane Katika Kukabiliana na Covid-19




Kundi la wanasayansi wa kimataifa linalojulikana kama -Viola Priesemann-limetoa wito kwa Ulaya kuungana katika kulitokomeza janga la virusi vya corona.
Katika andiko lao lililochapishwa na jarida la kitabibu "The Lancet medical Journal" wamesema kwa zingatio la mipaka ya nchi hizo iko wazi, itakuwa vigumu kwa taifa lolote kuweza kushusha viwango vya maambukizi pasipo umoja.

Aidha wameonya kwamba endapo hakutakuwa na hatua zitakazochukuliwa kwa sasa, kutegemewe mawimbi mengine ya maambukizi katika siku zijazo, ambayo yatakwenda sambamba na athari za kiafya, jamii, ajira na biashara.

Wamependekeza hatua madhubiti kwa mataifa hayo kupunguza idadi ya maambukizi mapya kwa kutopindukia watu 7 kwa jumla ya 100,000, kwa kila wiki katika kila nchi barani kote.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad