Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, ameiagiza Tume ya Maadili, kuhakikisha kwamba taarifa zinazojazwa na watumishi wa umma haziwekwi mtandaoni kwani kufanya hivyo inaondoa usiri wa taarifa hizo na kuwapa nafasi kubwa wadukuzi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Desemba 24, 2020, mara baada ya kumuapisha Kamishna wa Maadili aliyemteua hapo jana, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, na kuongeza kuwa fomu hizo zipakuliwe mtandaoni na kisha mhusika azijaze na kuzipeleka mahali sahihi.
"Nilitoa observation ya zile fomu zenu ambazo mmekuwa mkizitoa kwa mtandao na mlisema ziwe zinarudishwa kwa mtandao, unaweza ukafanya katoa mambo yote kwa mtandao, lakini kwa mfano Katibu Mkuu Kiongozi aeleze alichonacho aseme ana nyumba ndogo aiweke kwenye mtandao ule usiri na utakatifu wa idara ile mnaupoteza", amesema Rais Magufuli.
"Ni lazima pawe na usiri wa fomu hizi, mtu akishajua ile progaram anaweza aka-editi, hackers (wadukuzi), wako wengi, umejaza una milioni 10 akakujazia milioni 100, halafu baadaye unaulizwa ulijaza Milioni 100 na sahihi yako hii hapa, msikubali kamwe kurudisha fomu hizi kwa njia ya mtandao", ameongeza Rais Dkt. Magufuli.