Kama Mzazi Unaambiwa Mtoto Anakuhitaji zaidi ya Vitu Unavyomnunulia na Kumpa

 


Jitihada na mipango katika kuhakikisha mtoto anapata malezi mema ni jukumu la mzazi na jamii kwa ujumla. Mzazi ndio muhusika mkuu wa jambo hili la ulezi na ukuzi, kwasababu mwisho wa siku lawama na kongole zitamuhusu yeye nasi mwengine.


Mtoto inabidi afundishwe adabu akiwa bado hajapevuka, ili atakapokuwa amefika kwenye hali ya kujitambua kimwili na kiakili awe kashapata misingi imara ya malezi ambayo itamfaa yeye na jamii yake. Siku zote tabia mpya huwa ni ngumu kuingia hasa ikiwa mtu kashapitia kwenye tabia nyengine kinyume na hiyo unayotaka awe nayo kwasasa.


Uzuri wa tabia njema unapomfunza mtoto akiwa bado hajapevuka huwa ni rahisi kuingia akilini mwake na kukutii kwa kile unachomueleza kwasasababu ubongo wake bado haujakomaa kiasi cha kushindwa kubadilika. Oprah winfrey ni mmoja kati ya watangazaji maarufu sana nchini marekani na kote duniani.


Katika kipindi chake cha "Oprah winfrey show" aliwahi kufanya mahojiano na familia moja ya kiyaudi inayoishi kusini mwa marekani. Akastajaabu sana kukuta watoto wa familia hiyo alioitembelea hawatizami kabisa Tv. Maisha yao ni kusoma sana vitabu kuliko kutizama vitu vyengine vya anasa.


Ulezi wa aina hii ndio utajenga kupatikana watoto makini katika jamii yetu. Hatusemi kuwa nawe ufanye kama familia hiyo ila unaweza kumuwekea misingi mtoto muda gani atizame tv na kipindi gani ili kumjenga mtoto vizuri kiakili na kimwili kwa ustawi wake na wako.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad