Zimekuwa ni siku chache ngumu katika Manchester United, huku maswali mengi yakiulizwa kumuhusu Ole Gunnar Solskjaer na wachezaji wake.
Hata hivyo neno kuu katika Old Trafford limekuwa ni moja tu -imani kuhusu mwelekeo wao , licha ya kwamba walitolewa katika michuano ya Ligi ya Championi Jumanne.
Na ujumbe huo umekuwa ukisisitiziwa na Ole Gunnar Solskjaer katika mikutano yake na waandishi wa habari kabla ya mechi ya leo na Manchester City.
” Mchezaji yeyote anapaswa kusikitika na kukanganyikiwa wakati anaposhindwa ,” alisema Solskjaer.
“Msimu huu tumeshughulikia mapungufu vizuri”.
“Kabla mchezo ujao, unapaswa kutathmini kile ambacho hakikwenda vizuri, lakini ni muhimu kutochanganyikiwa kila mara kwasababu unafahamu katika soka huwezi kushinda kila mechi.
“Lakini kuna mechi utakazoshindwa ambazo utaumia zaidi kuliko nyingine baadhi ya zile utakazoshindwa zina athari zaidi kuliko nyingine.
“Ukweli ni kwamba tuko nje ya Championi Ligi kwa kipindi kilichobakia cha msimu. Lazima tusonge mbele na kurejea tena tena katika Championi Ligi.”