Kenya 'yaagiza dozi milioni 24 ya corona'



Kenya ameagiza dozi milioni 24 ya chanjo ya Covid-19, kwa mujibu wa Gazeti la The Star limeripoti, likiwanukuu maafisa wa wizara ya afya.
Serikali ya Kenya itatumia shilingi bilioni 10 sawa na($89m; £66m) kununua chanjo hiyo, gazeti hilo linaripoti.

Wizara iliwasilisha ombi lake lake kwa Mpango wa Ushirikiano wa Chanjo Duniani (Gavi) wiki iliyopita, kwa mujibu wa ripoti.

Hii itawafikia asilimia ya 20 ya idadi ya watu nchini humo.

Benki ya Dunia inakadiria kuwa Kenya wa sasa ina zaidi ya watu milioni 52.

Haijabainika ni chanjo ipi iliyoagizwa na nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kati kati ya mwaka huu Gavi ilisema kila dozi ya Covid-19 itagharimu $3.

Waliorodheshwa kupewa chanjo ni wahudumu wa afya, wazee na wale waliyo na changamoto zingine za kiafya

Gavi imetia saini mkataba na makampuni karibu tisa ya utengenezaji chanjo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad