Kimbunga cha theluji chasumbua utoaji wa chanjo ya COVID-19 Marekani




Theluji kubwa inaendelea kuangua kaskazini mashariki mwa Marekani, ikitatiza shughuli za kusafirisha na kutoa chanjo ya COVID-19 zilizoanza siku chache zilizopita nchini humo. 

Kimbunga hicho cha theluji kilianzia jimboni Virginia na kuenea hadi New England jana Jumatano, katika baadhi ya maeneo ikiwa na kina cha sentimita 60 leo Alhamisi. 

Hata hivyo, maafisa wa usambazaji wa chanjo wamesema hawatarajii kuwa theluji hiyo itatatiza pakubwa kazi yao. 

Waziri wa afya wa nchi hiyo Alex Azar amesema maafisa wa serikali wanafuatilia hatua kwa hatua usafirishaji wa chanjo na wafanyakazi wamewasili katika vituo wanakohitajika, na kuongeza kuwa anaamini kampuni zinazoisafirisha chanjo hiyo zina uwezo wa kukabiliana na vimbunga vya theluji. 

Watabiri wa hali ya hewa wamesema kimbunga kikali zaidi cha theluji kinasubiriwa katika jimbo la Pennsylvania, ambacho kinahofiwa kuvunja rekodi ya theluji iliyowahi kuanguka jimboni humo kwa miaka sitini iliyopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad