Kocha wa Simba Ataja Sababu za Kumuacha Bongo Morrison, Wadau Waanza Kusema Hana Jambo Simba


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa nyota wao ambao wamebaki Bongo ni mpango na mbinu ya kiufundi kwa ajili ya mechi zijazo.


Miongoni mwa nyota ambao watakosekana kwenye mchezo wa leo ni Bernard Morrison mwenye bao moja na pasi mbili kiungo mshambuliaji wa Simba atakosekana kwenye mchezo wa Leo Desemba 13 dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.


Morrison hakusafiri na timu ambayo ilikwea pipa Desemba 11 kuwafuata wapinzani wake ambao watakutana leo Uwanja wa Sokoine.


Mbali na Morrison nyota wengine ni Ibrahim Ajibu mwenye bao moja na pasi mbili za mabao Charles Ilanfya, Kenedy Juma ambao wamepewa program na Sven Vandenbroeck huku Larry Bwalya mwenye pasi moja ya bao yeye ana matatizo ya kifamilia.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa sababu ya kuwakosa nyota hao ni kutokana na mpangilio wa ratiba ili wawe bora zaidi.

"Kuna wakati inabidi umpumzishe mchezaji ili awe bora kwenye mechi ijayo au kama sehemu ya mpango wa mbinu na ufundi,".

Kwa upande mwingine mtaani wadau wa soka wanadai Bernad Morrison amejichimbia kaburi kwenda simba kwani umaarufu wake umeisha na hata soka achezi vizuri kama ilivyokuwa Yanga 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad