Luis Agomea Mamilioni ya Waarabu




MEBAINIKA kuwa winga machachari wa Simba, Luis Miquissone ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa ana furaha na hana mpango wa kuondoka ndani ya timu hiyo licha ya kuhitajika na matajiri wa Kiarabu kutoka nchini Misri, timu ya Pyramids.

 

Timu ya Pyramids hivi karibuni ilitajwa kuwa ipo tayari kuvunja mkataba wa winga huyo ulio na thamani ya Sh bilioni 1.3, ambapo Waarabu hao walikuwa tayari kutoa kiasi cha Sh bilioni 1.5 ili kumsajili winga huyo machachari.



Akizungumza na Championi Jumatano, mmoja kati kiongozi wa Simba ambaye jina lake hakutaka kutajwa, alisema kuwa kikao ambacho walikaa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji na Luis walikuwa wakijadili juu ya dili hilo ambapo winga huyo aliuambia uongozi kuwa ana furaha kuendelea kuitumikia Simba na wala hana mpango wa kuondoka ndani ya timu hiyo.“

 

Unajua suala la mchezaji Luis Miquissone na wale Waarabu wa Misri ni suala ambalo lipo, Waarabu walishaleta hiyo ofa na ndiyo maana utaona kulifanyika kikao cha bosi mkubwa na Luis na kikao kilikuwa kinazungumzia hilo dili ambalo lililetwa mezani, hivyo bosi alikuwa akimtaarifu Luis juu ya uwepo wa dili hilo“

 

Kwa upande wa Luis baada ya kupewa taarifa hizo na bosi yeye inadaiwa alimuambia bosi kuwa ana furaha ya kuendelea kuichezea Simba kwa misimu mingine zaidi huku akisema kuwa hana mpango wa kuondoka ndani ya timu hiyo,” alisema kiongozi huyo.

NA Marco Mzumbe, Dar es Salaam
 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad