Staa wa muziki nchini, msanii Lulu Abbas @luludivatz ambaye kwa sasa anafanya vizuri kupitia video ya ngoma yake, "Hauna Maajabu", amefunguka kuhusu hatua ya wasanii wawili wa kike nchini, #VanessaMdee na #Jolie kuacha muziki.
Akizungumza na XXL ya CloudsFm, @luludivatz amesema kuwa muziki ni mgumu sana na wasanii wa kike wanapitia changamoto nyingi.
“Muziki ni mgumu sana, hakuna kitu kirahisi katika dunia hii, hata anayeuza mwili ni ngumu kwa sababu kutembea na kila mwanaume ili upate fedha pia ni shughuli pevu,” amesema.
“Sisi watoto wa kike mioyo yetu ni milaini sana, kwa hiyo kuna muda unachoka, sio wao tu hata sisi jua linatuwakia,” amesema @luludivatz.
Ikumbukwe, ni takribani miezi mitatu sasa tangu Vanessa Mdee kutangaza kuachana na muziki, huku ukiwa ni mwezi mmoja pekee tayari umepita, Jolie kuweka wazi kuacha muziki.