KAMA mambo yakienda sawa basi aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Mzambia George Lwandamina
atamwaga saini ya kubeba mikoba ya Mromania Aristica Cioaba ndani ya kikosi cha Azam FC.
Lwandamina anapewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Cioaba Lwandamina atajwa kutua Azam FC kutokana na kocha kuwa hana timu ya kuifundisha baada ya kuachana na Zesco United mwezi Septemba mwaka huu.
Taarifa ambazo Championi Jumatano, limezipata ni kuwa mabosi wa Azam FC wanamtazama Lwandamina aliyetwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Yanga kwa ajili ya kuja kuifundisha timu hiyo kwa msimu huu.
“Kuna orodha kubwa lakini nafasi ipo kwa Lwandamina kwa sababu alifanya vizuri hapa ikiwemo kutwaa ubingwa wa ligi kuu, “Kwa hiyo mchakatounaendelea na kama kila kitu kitaenda sawa basi si ajabu kocha huyo akaja kwa sababu kwa sasa yupo kutokana na kutokuwa na timu ya kuifundisha,” kilisema chanzo hicho.
Championi Jumatano, lilimtafuta Msemaji wa Azam FC, Thabith Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ambapo alisema: “Hilo suala lipo kwa viongozi wa wa juu lakini kwa sasa wanatajwa makocha wengi kuja hapa ila hatuna haraka sana na suala hilo kwa sababu timu ipo chini ya kaimu kocha mkuu Vivier Bahati.”