Maalim Seif: Nisiitwe msaliti kukubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar



Unguja. Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa ACT-Wazalendo na yeye kuridhia kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitafa Zanzibar (SUK) usitafsiriwe kuwa ni usaliti kwa wananchi.


“Eti wapo wanaosema mimi ni msaliti kwa kukubali kuingia katika Serikali. Kilichotokea si uamuzi yangu, bali ni uamuzi ya wananchi pamoja na kamati kuu. Mimi kama kiongozi mkuu wa chama kazi yangu ni kusimamia na nitaendelea kufanya hivyo kwa maslahi ya Wazanzibar,” alisema Maalim,


Desemba 8, 2020 Maalim Seif alikula kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kuja na uamuzi wa kuingia katika Serikali hiyo.


Hatua hiyo iliwagawa baadhi ya wapenzi, wafuasi na wanachama wa chama hicho, huku kwa nyakati tofauti Maalim Seif na Dk Mwinyi wakieleza mikakati ya Zanzibar mpya, wakisisitiza maslahi mapana ya nchi hiyo.


Awali, chama hicho kilipinga mwenendo na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, kikidai kuwepo kwa matukio ya wanachama wake kuuawa na kuteswa.


Jana, Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo alizungumza katika mkutano uliofanyika makao makuu ya chama hicho Vuga Mjini Unguja na kukanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba yeye ni msaliti wa Wazanzibar kwa kukubali kuingia katika Serikali hiyo.

 

“Nani nimemsaliti mimi?” alihoji Maalim Seif aliyesema kuwa suala hilo waliwahoji wananchi walipofanya ziara na wapo waliotaka wasiingie kwenye SUK, japo waliokubali walikuwa wengi.


Kuhusu watu aliodai kuwa wanajifanya kuwa wanachama wa ACT Wazalendo wakidai kukihama chama hicho kutokana na hatua hiyo, aliwataka waondoke. “Anayetaka kwenda CCM na aende, anayetaka kwenda Chadema na aende, anayetaka kwenda NCCR-Mageuzi na aende, wanaoumia na chama chao wapo na wapo tayari kukulinda ili kiendelee,” alisema.


Maalim Seif alisema kwa sasa hakuna mbadala,bali ni kukubali kufanya kazi na Dk Husein Mwinyi katika kuiletea maendeleo Zanzibar na kuondosha chuki baina ya wananchi wake.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ulicho fanya Maalim ni Busara na Hekma kwa Maslahi mapana ya Zanzibar na Wazanzibari.

    Fatuma aende kwa Ubelijigi.

    Wasaliti wana kwao, huko Belijiggi. wewe uko nasi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Seif Sharif, wewe ni makamu, huyu anaesema wewe ni tissue , ana wivu na wewe. kwanza chama chake ni kingine, yeye ameondoka nchini na kukimbia kesi mahkamani Kisutu.

      Unafikiri angeipata hii nafasi, angemwachia Mbowe.?

      Maalim, Chapa Kazi msaidie Rais Minyi Zanzibar iende mbele...ZANZIBAR MPYA.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad