Mahabusu aliyempaka polisi kinyesi na kutoroka anaswa

 


Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Bura, kaunti ya Tana River nchini Kenya wamefanikiwa kumkamata mfungwa, Abdul Awadhi(19) aliyetoroka jela baada ya kumpaka kinyesi Afisa wa polisi.


Awadh alikamatwa jana yJumatano, Disemba 2, akiwa safarini kuelekea eneo la Nanighi huku akitumia vichochoro ili kukwepa polisi.


Akithibitisha kukamatwa kwake, Afisa Msimamizi wa kituo cha Bura, Benedict Mwangangi, amesema Awadh alikuwa amezuiliwa kwenye selo ya polisi kwa tuhuma ya kushambulia na kujeruhi kabla ya kutoroka kwake mnamo Jumatatu, Novemba 30.


“Alipaswa kufikishwa mahakamani Desemba 10, hivyo tulikuwa tumemzuia huku tukiendelea na uchunguzi,” Mwangangi 


Imeelezwa kuwa, Awadh aliomba ruhusa kwenda msalani na alisindikizwa na Anthony Wanjau lakini alichukua muda mwingi chooni jambo ambalo lilimtia Wanjau wasiwasi na ni wakati alipomuamuru aondoke ndipo alimrushia kinyesi usoni na kutoroka.


"Mshukiwa alikawia msalani na wakati afisa huyo alipokaribia mlango kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea, alitoka nje ghafla na kumpaka Afisa huyo kinyesi usoni kabla ya kuchanja mbuga," ripoti ya polisi imeeleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad