Mahakama Ujerumani kutoa hukumu ya shambulizi la Halle




Mahakama ya Ujerumani leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi inayomkabili mfuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia aliyeshambulia sinagogi wakati wa sikukuu ya Kiyahudi ya Yom Kippur na kuwaua watu wawili baada ya kushindwa kuingia ndani. 
Shambulizi hilo la Oktoba 9, mwaka 2019 linachukuliwa kama moja ya mashambulizi mabaya ya uhalifu dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani katika historia ya baada ya vita. 

Mshtakiwa Stephan Balliet, mwanaume mwenye umri wa miaka 28 anadaiwa kuchapisha maneno ya chuki dhidi ya Wayahudi kabla ya kujaribu kushambulia sinagogi kwenye mji wa mashariki mwa Ujerumani, Halle, huku akilionesha mubashara shambulizi hilo kwenye tovuti maarufu ya michezo. 

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wameitaka Mahakama ya jimbo la Naumburg karibu na Magdeburg kumhukumu Balliet kwa mauaji, jaribio la mauaji, kuchochea chuki na jaribio la kutoa kitisho.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad