Chuo cha Sanaa cha Ufaransa kimesema Pierre Cardin, mbunifu wa Kifaransa ambae ni miongoni mwa waliotamba katika ulimwengu wa mitindo wakati wa karne ya 20, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98.
Kwa kutumia ubunifu, Cardin, alitengeneza bidhaa mbalimbali kuanzia saa za mkononi hadi mashuka ya vitandani na kufanya nembo yake kuwa moja kati ya maarufu zaidi duniani.
Bidhaa za chapa yake ziliuzwa zaidi katika miaka ya 1970 na 80, ingawa kiwango hicho kilishuka pia kwa kiwango kikubwa katika miongo ya baadae.