Mganga Atimuliwa kwa Tuhuma za Kubaka Wagonjwa



MGANGA wa tiba za asili (kienyeji) anayefahamika kwa jina la Kambo Kilima (78) ambaye makazi yake hayajafahamika anatuhumiwa kubaka wagonjwa wawili aliokuwa akiwatibu baada ya wagonjwa hao kufika kwenye kambi yake aliyoianzisha mpakani mwa wilaya ya Kyela na Makete.

 

Awali imeelezwa kuwa Mganga huyo anayetumia ‘biblia’ katika kutazama matatizo ya wagonjwa, aliweka kambi katika moja ya kijiji kilichopo kata ya Matema wilayani Kyela lakini alifukuzwa baada ya kutuhumiwa kumbaka mgonjwa aliyekuwa akimtibu.

 

Baadhi ya wakazi wa kata hiyo, waliozungumza na UWAZI walisema kuwa ilimlazimu mganga huyo kuhamia kwenye safu za milima iliyopo kijiji cha Ngyekye kuelekea Makete.

 

Hata hivyo, AMANI baada ya kupata taarifa hizo na kuanza kufunga safari kumfuata hakuweza kupatikana kwani alikuwa tayari ametokomea kusikojulikana.

 

Wakazi hao wanaoishi mpakani mwa Kyela na Makete katika kijiji cha Igeni akiwamo David Mwamaja alisema walimuona mtu huyo akiwa na mabegi akielekea upande wa kaskazini mwa mlima huo ambapo bado haijajulikana anakokwenda kuweka kambi na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

STORI; IBRAHIM YASSIN, Mbeya


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad