Miili 20 ya Wahamiaji Yaopolewa Pwani ya Tunisia

 


Miili 20 ya wahamiaji kutoka ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara, imeopolewa leo katika pwani ya Tunisia baada ya boti yao kuzama. 

Msemaji wa jeshi la Tunisia Mohamed Zekri amesema hayo. Zekri ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wahamiaji wengine watano waliokolewa na kuongeza pia kuwa operesheni ya uokozi inaendelea. 


Hakutoa maelezo zaidi kuhusu mkasa huo aliyosema ulitokea pwani ya Sfax eneo la kati nchini Tunisia. 


Tunisia ambayo iko maili chache tu kutoka Ulaya, imekuwa ikitumika kwa muda mrefu na wahamiaji wanaovuka kwenda Ulaya kwa njia isiyo halali. 


Kulingana na wizara ya ndani ya Tunisia, kati ya mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu jumla ya wahamiaji 8,581 wamezuiwa nchini humo wakati wakijaribu kuvuka bahari Mediterrania kuelekea Ulaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad