Mkenya alieshiriki njama tukio la September 11 apelekwa New York





Mshirika wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab anayeshutumiwa kula njama kufanya shambulizi la mtindo wa Septemba 11 nchini Marekani amepelekwa New York kukabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Raia huyo wa Kenya Cholo Abdi Abdullah alihamishwa Jumanne kutoka Ufilipino ambako alikuwa chini ya ulinzi wa askari wa huko tangu alipokamatwa July 2019. Ufilipino ilimkabidhi kwa Maafisa wa Marekani Jumanne.

Abdullah anatuhumiwa kwa kula njama za kutaka kuteka ndege ya abiria na kuiangusha kwenye jengo moja nchini Marekani ikiwa ni sehemu ya njama iliyoongozwa na viongozi wakuu wa al-Shabaab, Abdullah anadaiwa kupata mafunzo ya urubani huko Ufilipino.

Alishtakiwa katika mashtaka sita yaliyofunguliwa Jumatano na alitarajiwa kufikishwa kwa Jaji wa Serikali kuu huko New York.

Mashtaka dhidi yake ni pamoja na kutoa msaada wa vifaa kwa taasisi ya ya kigaidi ya kigeni na kula njama za kuua raia wa Marekani na njama za kuteka nyara na kuharibu ndege.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad