Msanii Ben Pol achaguliwa kuwa kwenye Baraza la Biashara Huru Afrika



MSANII Behnam Paul ‘Ben Pol’ ndiye Msani pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki aliyechaguliwa kushiriki Baraza la biashara huru Afrika AfCFTA nchini South Africa leo, ambalo litahudhuriwa na wakuu wa nchi 55. Biashara huru Afrika inaanza rasmi Januari mosi mwaka 2021 na itawezesha nchi za Afrika kufanya biashara bila vizuizi.



Akizungumzia uteuzi huo Pol alisema kuwa ana mshukuru Mungu kupata nafasi hiyo na anajivunia kuiwakilisha Tanzania na Afrika Mashariki na kati katika baraza la African huru la Biashara Afrika ambalo linafanyika leo, likiongozwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais Paul Kagame (Rwanda) na wakuu wa nchi 55, CEO’s mbalimbali kutoka sekta binafsi, Wanamichezo na Wadau mbalimbali kutoka Afrika.

“Januari 2021 Afrika itaanza rasmi kufanya biashara na Afrika, yaani soko la nchi za ndani lenye watu Bilioni 1.2 na thamani ya dola trilioni 2.5 ikijumuisha mataifa 55.

Huu ni wakati wa Kihistoria sana kwa bara letu. Mungu ibariki Afrika. Asante sana African Union (AU), Hongera na Asante Afrika na Msanii pekee Tanzania ma Afrika mashariki niliyechaguliwa kushiriki baraza la biashara huru Afrika AfCFTA nchini Afrika Kusini leo “alisema Ben Pol.

“Namshukuru Mungu na ninajivunia kuiwakilisha Tanzania na Afrika Mashariki katika Baraza la AfCFTA (African Continental Free Trade Area) leo ijumaa 04.12.2020 nchini South Africa, baraza ambalo litahudhuriwa na wakuu wa nchi 55, AfCFTA (African Continental Free Trade Area) itaanza kwa vitendo Januari 1, 2021 na itazifanya nchi za barani Africa kufanya biashara huru bila vikwazo.

Huu ni wakati wa Kihistoria kwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad