Muuaji Hatari Nchini Marekani Afariki Dunia




SAMUEL LITTLE, mtu aliyetajwa na shirika la upelelezi  la Marekani (FBI) kama muuaji mkubwa wa kuvizia katika historia ya Marekani,  amefariki akiwa na umri wa miaka 80.

 

Little alifariki katika hospitali mjini California siku ya Jumatano, idara ya magereza imesema. Alikuwa akitumikia kifungo cha mauaji ya wanawake watatu. Lakini kabla ya kifo chake alikuwa amekiri kuwaua wanawake 93 kati ya mwaka 1970 na 2005.

 

Mtu huyo aliwalenga watu waliokuwa hawawezi kujitetea, wengi wao wakiwa makahaba ama watumiaji wa mihadarati, walisema maafisa.

 

Alikuwa akiua bila kuacha ishara zozote za mauaji, kama vile kuwadunga kisu ama kuwapiga risasi.

 

Badala yake,  vifo vingi alivyohusika, vilidaiwa kuwa ni vya kula madawa ya kulevya kupitia kiasi ama vya ajali na havikuchunguzwa. Baadhi ya miili haijapatikana hadi leo, kitengo hicho kilisema.

 

Mwaka uliopita, FBI lilisema kwamba wachambuzi wake walisema kwamba madai yote aliyokiri kutekeleza yalikuwa ya kweli. Pia, walitoa picha za waathiriwa aliowachora wakati akiwa jela katika jaribio la kuwatafuta aliowaua.

 

Shirika la FBI lilitoa michoro ya Samuel Little kwa matumaini kwamba waathiriwa watatambulika.  Little alikamatwa mwaka 2012 kwa mashtaka ya kutumia mihadarati mjini Kentucky na kusafirishwa hadi California ambako maafisa walitafuta vinasaba vyake.

 

Tayari alikuwa na rekodi mbaya ya uhalifu akiwa na mashtaka ya wizi wa kutumia nguvu hadi ubakaji katika maeneo mbalimbali Marekani. Vinasaba vya DNA vilimhusisha na mauaji ya watu watatu ambao hayajatatuliwa kutoka 1987 na 1989 katika kaunti ya mji wa Los Angeles.

 

Alikana kufanya makosa hayo lakini hatimaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha bila fursa ya kuachiliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad