Rais Nana Akufo Addo achaguliwa tena kuwa Rais Ghana
12/10/2020 08:00:00 AM
Rais Nana Akufo Addo, wa Ghana ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa kupata asilimia 51.6 ya Kura, dhidi mpinzani wake wa karibu, Rais wa Zamani wa taifa hilo, John Mahama aliyepata asilimia 47.4 ya kura zote.
Rais Akufo Addo ametetea nafasi yake hiyo,dhidi ya mpinzani wake huyo ambaye tangu awali alionyesha wasiwasi wake wa kutumika kwa nguvu ya Jeshi kwenye uchaguzi huo.
Bwana Mahama amelalamikia wizi wa kura. Akiongea muda mfupi baada ya tangazo hilo, Rais Akufo Addo amewashukuru raia kwa kumchagua.
"Nimeguswa tena sana na kuaminiwa nanyi na sichukulii hili kuwa jambo dogo...labda ipo tabia ya kuwa rais aliyepo madarakani akichaguliwa tena muhula wa pili anachukulia hilo kiurahisi na kuanza kupumzika ...lakini mimi ni wa tofauti.
Ninawashukuru sana , Waghana wenzangu kwa ushindi huu".
Awali polisi walisema kulikuwa na kesi 21 wakati wa uchaguzi huo zinazohusiana na ghasia tangu Jumatatu, huku watu watano wakiwa wamefariki
Huu ni uchaguzi wanane wa urais tangu katiba ilivyoandikwa mwaka 1992.
Former Ghanaian President and candidate of the opposition National Democratic Congress (NDC) John Dramani Mahama
Aidha rais Akufo Addo aliongeza kusema kuwa kazi ya dharura ambayo ataendelea kuifanya ni kuendelea na mchakato wa kugeuza athari ambazo Covid 19 imekuwa nazo katika uchumi na maisha ya kila siku.
Jambo la muhimu ni kuliweka taifa katika njia kamili ya kufufua uchumi na maendeleo.
Kabla ya janga hili, mkikumbuka Ghana ilikuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi duniani na ninawahakikishia tutapata sifa hiyo tena," rais wa Ghana alisisitiza.