Mwimbaji wa Nigeria Omah Lay amefunguka kwa mara ya kwanza sakata lake la kukamatwa nchini Uganda. Amesema alichukuliwa kama Jambazi sugu kipindi yupo rumande.
Omah Lay na mwimbaji mwenzake Ms. Tems walikamatwa na kufikishwa mahakamani wakishtakiwa kwa makosa ya kukiuka kanuni za COVID-19 nchini humo mara baada ya kufanya onesho la muziki mnamo (Dec. 13)
Kwenye mfululizo wa tweets zake Omah Lay ambaye tayari ameachiwa huru na kurudi Nigeria, amesema "Siku chache zilizopita zimekuwa ni siku ngumu sana katika maisha yangu. Nilikuwa kwenye nchi yenye watu wazuri, kilichofuata ni kuchukuliwa kama jambazi sugu." ilisomeka tweet ya Omah Lay.
"Pia nataka kutoa ufafanuzi wa sakata hili, kabla ya kuja Uganda, Ma Promota walithibitisha kwamba wamehakikisha kila kitu kipo sawa na vibali vyote ikiwemo kanuni za COVID-19"
"Kwa hatua hiyo, wajibu wangu ulikuwa ni kufika na kuwa tayari kupelekwa kwenye ukumbi na kuburudisha, kitu ambacho nilikifanya kwa uangalizi wa polisi."