Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Andrea Kundo amesema Wizara yake itaacha kukumbatia teknolojia za nje na badala yake itawasaidia wataalamu wa ndani ili waweze kujiongezea kipato.
Naibu Waziri amesema ni lazima Programu za mitandao ya kijamii za Whatssup na Instagram ziwasaidia watanzania kujiongezea kipato.
Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kukutana na wafanyakazi wa Wizara hiyo, Naibu Waziri huyo amesema Wizara yake itaanza kuwawezesha wataalamu wa ndani ili kukuza teknolojia ambayo itawasaidia kukuza uchumi.
“Lazima tuhakikishe teknolojia yetu inakuwa, huwezi kuwa na kiwanda cha sukari halafu unaagiza zaidi kutoka nje maana yake cha ndani hakiwezi kufanya vizuri, maana yake ni kwamba sisi Serikali, sana sana Wizara hii tusiende kuwa namba moja kukumbatia teknolojia za nje twende tuje na kuhakikisha tuna platform na wataalumu wetu,” Kundo
Vilevile, amesema programu za mitandao ya kijamii za Whatsupp na Instagramu zinatakiwa kuwaongezea kupato watanzania.
“Mfano Whatsapp ni Programu hivyo tukiwa na Programu yetu tunaweza kutengeneza platform ambayo itajibu mahitaji yale yale lakini ikiwa yanatokana na Nchi yetu, lakini pia Programu kama vile Instagram ni Platform ya kibiashara iwapo wataalamu wetu watapewa uwezo wataweza na tutapata kodi na tutaweza kuwa na uses na usalama wetu utaimarika zaidi,” Kundo