Polisi aliyemuua raia wa Kiafrika afutwa kazi Marekani




Afisa wa polisi aliyehusika na mauaji ya raia mwenye asili ya Kiafrika amefutwa kazi katika mji wa Columbus, jimbo la Ohio nchini Marekani.
Mkurugenzi wa Usalama wa Umma wa Columbus Ned Pettus, alitoa taarifa kuhusu mauaji ya Andre Maurice Hill mwenye umri wa miaka 47 na asliye na asili ya Kiafrika, yaliyotekelezwa na polisi mnamo Desemba 21.

Pettus alitangaza kwamba afisa wa polisi Adam Coy, ambaye alimuua Hill, alifutwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu na uzembe.

Akibainisha kwamba Hill pia alicheleweshwa kupewa huduma ya kwanza, Pettus alisema,

"Kitendo cha Hill kufyatuliwa risasi,  ni janga kwa jamii yetu na polisi, na kwa mtu yeyote anayempenda."

Pettus aliongezea kusema kuwa vitendo vya Coy havikidhi kiapo cha polisi wala kuendana na vigezo  vya polisi vya Columbus.

Coy alisimamishwa kazi wiki iliyopita kama sehemu ya uchunguzi ulioanzishwa dhidi yake, na kesi ya kiutawala ilifunguliwa dhidi ya maafisa wengine katika eneo la tukio.

Hill, ambaye alikuwa katika karakana yake ya nyumbani, alifyatuliwa risasi na polisi na kufariki papo hapo.

Kulingana na kamera ya polisi, maafisa walipofika eneo la tukio, Hill alionekana akielekea kwa maafisa wenzie na simu yake ya rununu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad