Pompeo ailaumu Urusi kwa shambulzii kubwa la mtandao





 Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo ameilaumu Urusi kwa shambulio kubwa la mtandao dhidi ya mashirika ya serikali ya Marekani. 
Akizungumza katika kipindi cha redio, Pompeo amesema Urusi imekuwa ikifanya majaribio kadhaa ya kudukua mifumo ya kompyuta ya idara ya usalama wa taifa nchini Marekani. 

Wataalamu wa usalama wanasema shambulizi lililofanywa linaweza kuruhusu wadukuzui kufikia mifumo ya kompyuta bila mipaka pamoja na mifumo muhimu ya serikali na huduma nyengine. 

Idara ya Usalama wa Taifa imewataka watumiaji wa mitandao kuwa makini ili kuzuia kudukuliwa kwa data za kijeshi na nyenginezo. 

Rais mteule Joe Biden ameelezea wasiwasi wake juu ya udukuzi huo huku Seneta wa Republican Mitt Romney akiilaumu Urusi kutumia fursa ya ukimya wa Marekani kuendesha uhalifu huo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad