Rais Magufuli Atunukiwa Tuzo

 




Uongozi wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly, kupitia Kamati Kuu na Halmashauri Kuu imemtunukia tuzo ya uongozi Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake, ambapo Tanzania chini ya uongozi wake imekuwa mfano wa kuigwa katika Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

 

Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumapili, Desemba 20, 2020 kwenye ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Kanisa la Philadelphia Gospel Assembly, Baba Askofu Dkt. Yohana Masinga iliyofanyika katika makao makuu ya kanisa hilo Area C Wajenzi jijini Dodoma.

 

“Ama kwa hakika hofu ya Mungu aliyonayo kiongozi wetu ndiyo hasa siri ya kufanikiwa kwa uongozi wake na Taifa letu kwa ujumla. Sote ni mashuhuda kwamba Tanzania chini ya uongozi wake imekuwa nchi ya mfano Afrika na Dunia kwa ujumla katika kupiga vita rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma sambamba na kurejesha nidhamu ya kazi ambayo ilikuwa imepotea katika ofisi za umma.”

 

Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha hivi karibuni dunia nzima imeshuhudia jinsi Tanzania ilivyomtanguliza Mungu wakati wa mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID19). “Tanzania hatukujifungia ndani kama mataifa mengine. Tuliendelea na shughuli zetu kwa imani kabisa tukijua yupo Mungu ambaye ndiye kinga na msaada wetu pekee.”

 

Waziri Mkuu amesema jukumu alilokabidhiwa leo la kuwa Askofu Mkuu wa Makanisa ya Philadelphia Afrika, Asia na sasa Marekani siyo jukumu dogo ni kazi inahitaji hekima kuu ili kuwaongoza watu hao wa mataifa hayo yote kiroho na kimwili, amempongeza kwa maono hayo makubwa ya kuanzisha kanisa ambalo hadi sasa linapotimiza miaka 30 limeweza kuenea ndani na nje ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad