Rais Kenyatta ametoa idhinisha kwa wizara ya afya kuendelea na kutafuta tiba ya virusi vya corona nchini China.
Uamuzi wa nchi hiyo unawadia wakati nchi za magharibi zinanunua karibu dozi bilioni 3.8 za chanjo ambazo zimebainika, kwa mujibu wa Kituo cha afya na Uvumbuzi wa 'Duke' Duniani.
"Covid-19 imerejea tena kwa kasi mno Kenya, maambukizi yanaendelea kuongezeka," Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema Jumatatu.
Rais wa China Xi Jinping mnamo mwezi Mei aliahidi kupatikana kwa chanjo iliyokuwa inafanyiwa majaribio kuwa itatolewa Afrika kwa gharama ya chini.
Wataalamu wamesema hatua hiyo itakuwa njia ya kupunguza shutuma dhidi ya nchi hiyo kuhusu namna ilivyokabiliana na janga la corona mapema mwaka huu.
Sasa hivi Kenya inafanya majiribio ya chanjo ya Astrazaneca kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Moja ya nchi nne zinazoshiriki majaribio ya chanjo ni pamoja na Misri na Morocco kwa chanjo moja wapo ya China.
Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa China kimesema nchi hiyo ina chanjo 5 ambazo zimeingia katika awamu ya tatu ya majaribio.
Hata hivyo, Kenya haijatoa data kuhusu hatua zilizopigwa kwa chanjo inayofanyiwa majaribio nchini humo.
Hadi kufikia sasa watu 80,000 wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya corona Kenya huku zaidi ya 1,400 wakifariki dunia kwasababu ya ugonjwa huo