Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier, amemkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi, barua iliyoandikwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwenda kwa Rais Magufuli, ambaye amempongeza kwa kuiwezesha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati.
Hayo yamejiri mara baada ya Waziri Prof. Kabudi, kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa nchini na kuongeza kuwa baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, kujikita katika uwekezaji mkubwa wa maeneo ya miundombinu na nishati pamoja na huduma za kijamii sasa serikali inalenga kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi.
Hongera kipenzi chetu JPJM, Safari tulio ianza kwa hatua moja sasa tuko mbali, tutafika tu. TUCHAPE KAZI KWELI KWELI
ReplyDeleteKila Balozi kwa nchi anazo wakilisha, ajipange na kukutana na Chamber of commerce / international trade Authorities wakiwemo Waffanya Biashara Maarufu wa Nchhi hizo kutafutia nchi masoko ya uhakika ya kila kitu kuanzia Nyama Na diary prod/Samaki/Maharage/Pilipili/ Mananasi/ Manjano/Tangawizi/Parachichi/Matope tope/Ndizi/Mkaa/Mawe ya Slabs/korosho/pamba/Choya/Chai/ na mengine mengi.
Baada ya hapo tunawapa mwaliko kutembelea nchi kiutalii na kuwakutanisha na mashirika na wafanya biashara na mabenki nchini. Lengo ni kuinua Nchi na Maisha ya Wananchi.
Kumbuka/Rejea Hotuba ya Mh Rais JPM ufunguzi wa bunge la 12
its a road map by itself , full of hope. Watekelezaji mnatakiwaa muitekeleze on ground reality. vinginevyo hujamuelewa JPM wetu na Kutumbua ni Halali yake..
Mtakao teuliwa mjipange hasa Biashara na sina Uhakika kama itakuja Wizara mpya ya Masoko ya kimataifa ambayo itakuwa na vitengo vitatu Biashara na nchi za Ghuba Kiaara /Asia /Ulaya / Amelika