Robert Lewandowski , msahambuliaji nyota wa Bayern Munich alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa Fifa huko Zurich na kuwashinda washindi wa miaka iliyotangulia ,Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji huyo kutoka Poland alifunga mabao 55 katika michezo 47 tu msimu uliopita na kuisaidia miamba ya Ujerumani Bayern Munich kunyakua mataji 3 katika msimu moja,yaani kombe la ligi ya Ujerumani,kombe la taifa na ligi ya mabingwa ulaya.
Lewandowski mwenye umri wa miaka 32, alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi, kombe la taifa na Ligi ya Mabingwa.
Mlinzi wa Manchester City Lucy Bronze alishinda tuzo ya mchezaji bora wa wanawake.
Washindi waliamuliwa na uteuzi kutoka kwa manahodha wa timu za mataifa na makocha wakuu, kura ya mtandaoni ya mashabiki na wawakilishi 200 wa vyombo vya habari.