Rusesabagina kushtaki kampuni ya ndege ya Ugiriki





Mkosoaji mkuu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye anazuiliwa gerezani kwa mashtaka ya ugaidi amesema ataishtaki kampuni ya ndege ya kibinafsi ya Ugiriki kwa kuongoza njama ya utekaji na kupelekwa kwake nchini Rwanda.
Paul Rusesabagina - ambaye jukumu lake wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 iliangaziwa katika filamu ya Hollywood ya Marekani kwa jina Hotel Rwanda - alikuwa akiishi mafichoni nchini Marekani na Ubelgiji.

Rusesabagina 'anaamrishwa cha kusema na mamlaka za Rwanda'

Anasema mnamo mwezi Agosti alikuwa amenuia kuzuru Burundi kwa shughuli za kanisa lakini ndege ya kibinafsi aliyokuwa ameabiri kwenda Dubai badala yake ilimpeleka Rwanda.

Kesi iliyowasilishwa mbele ya mahakama mjini Texas inadai kuwa kamuni ya ndege hiyo , GainJet, alikubali kufanya safari hiyo kutokana na uhusiano wa karibu kati yak e na maafisa wa Kigali.

Kesi sawa na hiyo inatarajiwa kuwasilishwa katika mahakama nchini Ubelgiji ambako Bw.Rusesabagina ana uraia wake.

GainJet haijajibu ombi la BBC la kupata tamko lake kuhusiana na madai hayo.


Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eheee, Makubwa..!!! Hivyo hii Ubejiji iko wapi..??
    Kila nikijalibu kuitafuta, hata siionagi nasikiaga pia yule
    mwakilishi mkazi wa mabelubelu ndio ameludigi kwao.

    Hivyo zao lao kuu ni kilimo kipi..?
    na Arizzi yao ina ukubwa zaidi ya Afilika mara ngapi..??

    Ina mito na mabonde.?? milima na bahali.??

    I
    Au iko sayali yya mbali kama pluto vile..??

    Mtujuze wasomi na wana sasa wa nchini twita na fezibuku

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad