Kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Msaikolojia Isaack Kimario amefunguka sababu zinazolepelekea wanaume kuwahi kufariki na kuacha wake zao pale wanapokuwa kwenye ndoa.
Kwanza Isaack Kimario amesema sehemu ya Ubongo ya wanawake imeumbwa kufikiria 'future' na kuwaza mambo yaliyopita hivyo ni tofauti kidogo na wanaume pia hufanya kazi haraka zaidi ya wanaume
Sasa akitaja sababu hizo ameeleza kuwa "Kulingana na Taasisi ya Kisaikolojia inaeleza kuna sababu ambazo zinasababisha wanaume kufa haraka zaidi ya wanawake na hilo limekaa kibaiolojia na kisaikolojia, sababu ya kwanza ni asili na homoni ambazo wanazo zinawafanya wasipate magonjwa kama ya moyo, ambazo homoni hizo sisi tunazikosa"
"Sababu nyingine ni wanaume kujiweka kwenye 'risk' kubwa ya kupata athari za afya, kwa mfano michezo ambayo tunacheza kama rugby au magari ni michezo ambayo inahatarisha uhai tofauti na michezo ya wanawake , risk hiyo husababisha kufariki haraka"
"Wanaume tunashindwa kudhibiti tabia fulani ambazo zinaweza kuathiri afya zetu na tabia hatarishi kama kuvuta sigara, kunywa pombe kupita kiasi, na madawa ya kulevya. Takwimu zinaonyesha wanaume ndiyo tunakuwa tunaathirika zaidi"
"Kingine ni wanaume kujifanya wapo juu ya wanawake, uwanaume huo tunaokuwa nao unatufanya tuone matatizo tunaweza kuyatatua wenyewe na hatuwezi kumwambia mwanaume mwenzetu au mwanamke inasababisha tufe kwa Stress au huzuni"