Ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani zinaeleza kuwa karibu taasisi mbili za serikali ya Marekani zimedukuliwa.
Udukuzi huo unadaiwa kufanywa na kundi moja linaloungwa mkono na serikali ya kigeni ambayo haikutajwa.
Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa nchini Marekani John Ullyot amesema serikali ya Marekani imepata taarifa kuhusiana na ripoti hizo na inachukua hatua zote muhimu kuwatambua wahusika na kusuluhisha mambo yoyote yatakayoibuka kutokana na hali hiyo.
Ripoti zinaarifu kuwa kundi hilo lililofanya udukuzi limeiba taarifa kutoka wizara ya fedha na biashara.
Haya yanakuja wiki moja baada ya kampuni ya usalama wa mtandaoni FireEye kusema ilikumbwa na tukio kama hilo ambapo wadukuzi waliiba vifa vyake muhimu vya kupima mifumo ya kompyuta ya wateja wake.