Teyana Taylor Afunguka Kuacha Mziki, Afunguka Makubwa Kuhusu Lebo yake

 


Sio kwa Vanessa Mdee pekee, mwimbaji Teyana Taylor ametangaza kuachana na muziki. Kupitia ukurasa wake wa instagram wikendi iliyopita, Teyana aliushtua ulimwengu kwa maamuzi hayo mazito.

Akiwa LIVE kwenye instagram akaunti yake, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alizitupa lawama zote kwa label yake G.O.O.D Music/Def Jam Records, kwa kudai kuwa wameshindwa kumpa mafanikio licha ya kujituma kwake kwa asilimia 110 kwenye miaka yote 10 chini yao.

Aliweka wazi kwamba aliwahi kuwaomba Def Jam wamuachie huru kwa zaidi ya mara 10 lakini waligoma kufanya hivyo. Kikubwa ambacho amewaomba mashabiki zake ambao wanataka atengue maamuzi yake ni kwamba amefanya hivyo kwa ajili ya afya yake ya akili, watoto pamoja na familia, hivyo waheshimu maamuzi yake;

"Nafikiri ni ubinafsi flani kusema 'vipi kuhusu mashabiki zako? Fanya kwa ajili ya mashabiki zako." alisema Teyana na kuongeza "Nimefanya uamuzi huu kwa ajili ya usalama wa afya ya akili yangu, lazima nifanye hivi kwa afya ya hisia zangu. Kwa ajili ya watoto wangu, ili niweze kubaki hai kwa ajili ya watoto wangu." alieleza Teyana Taylor

Uamuzi wake umewagusa wengi akiwemo The Game ambaye amemtaka Teyana Taylor kuendelea kusonga mbele, huku Cardi B akimwaga sifa na akidhihirisha kwamba album ya 'The Album' ndio album bora kwa mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad