Twitter imethibitisha kwamba mamilioni ya wafuasi wa akaunti rasmi ya rais wa Marekani watafutwa kabla ya akaunti hiyo kukabidhiwa utawala wa rais mteule Joe Biden.
Timu ya bwana Biden 'iliping'a mpango huo huo lakini kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilisema kwamba uamuzi wake 'haubadiliki'.
Hatua hiyo inaashiria mabadiliko kutoka kwa utawala unaoondoka. Twitter ilikubali ombi la rais Donald Trump 2016 kuwarithi mamilioni ya wafuasi wa Barrck Obama.
''Mwaka 2016, utawala wa rais Trump uliwarithi wafuasi wote wa rais Obama katika akaunti ya @POTUS na ile ya @Whitehouse'', Rob Flaherty, mkurugenzi wa masuala ya mtandaoni alisema katika ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumatatu.
''Mwaka 2020 , Twitter ilituarifu kwamba utawala wa rais Biden utalazimika kuanzia sufuri''.Inaathiri wafuasi wa akaunti zinazomilikiwa na serikali kama vile @POTUS na @FLOTUS.
Twitter ilisema kwamba wale wanaomfuata rais aliyepo madarakani wataarifiwa kwamba wanawekwa katika kumbukumbu , na watapatiwa chaguo la kufuata akaunti ya utawala mpya wa Biden.
Akaunti ya kibinfasi ya bwana Biden @Joe Biden , ina wafuasi milioni 21.7 na haitaathiriwa ha hatua hiyo mpya.
Rais Trump amekuwa akitumia akaunti zake za Twitter rasmi na kibinafsi kuzungumza na wapigaji kura. Wakati wa utawala wake katika Ikulu ya Whitehouse amechapisha zaidi ya jumbe 50,000.
Hatahivyo ukweli ni kwamba tovuti inayofuatilia jumbe za twitter na akaunti za wafuasi tangu mwezi Novemba , inasema kwamba bwana Trump alipoteza wafuasi 369,849 katika akaunti yake binfasi tangu mwezi Novemba.
Wakati huohuo, rais mteule Joe Biden amejiongezea wafuasi 2,671,790. Hatua hiyo kutoka Twitter inajiri siku chache baada ya afisa mkuu mtendaji Jack Dorsey kuondoa ufuasi wake kwa rais Trump, bwana Joe Biden na makamu wa rais mteule Kamala Harris.
Mtaalamu wa masuala ya soko Rebecca Lodge kutoka kampuni ya Start Up Disruptors alisema kwamba uamuzi huo wa Twitter: Huku mamilioni ya watu wakiwa wafuasi wa akaunti moja mbali na kwamba wafuasi wa Donald Trump wana ushabiki mkubwa wa kiongozi huyo, huenda ni mpango wa Twitter kuhakikisha kwamba jumbe zozote zenye nia mbaya zinapunguzwa makali kabla ya rais mpya kuchukuwa mamalaka.