Uganda yasitisha kampeni za uchaguzi jijini Kampala


Uganda imesitisha kampeni zote za uchaguzi wa urais katika mji mkuu wa Kampala na wilaya nyingine 10 zenye idadi kubwa ya watu. 

Msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Paul Bukenya, amesema sababu ya kufuta kampeni ni ongezeko la maambukizo ya virusi vya corona. Hata hivyo wakosoaji wanadai sababu halisi ni umaarufu wa upinzani katika maeneo hayo. 


Taifa hilo la Afrika Mashariki limepanga kufanya uchaguzi wake mkuu Januari 14. Uganda imeshasajili watu 33,360 walioambukizwa COVID-19 na vifo 254 kutokana na ugonjwa huo. 


Mgombea wa upinzani na mwanamuziki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ameibuka kuwa mshindani mkuu wa Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986. 


Bobi Wine ni maarufu miongoni mwa vijana. Mwezi uliopita watu watatu walifariki katika ghasia zilizozuka baada ya polisi kumkamata Bobi Wine.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad