Uongozi wa KMC Watoa Neno Kuhusu Penalti ya Simba Yenye Utata Mkubwa



UONGOZI wa KMC umesema kuwa maamuzi ya penalti iliyotolewa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, Desemba 16 hayapo mikononi mwao kwa kuwa hiyo sio kazi yao.

Wakati ikiyeyusha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba, bao hilo lilipatikana kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 baada ya mwamuzi wa kati Elly Sassi kutafsiri kwamba mchezaji wa KMC aliunawa mpira huo.


Bao la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 77 na na kuifanya timu hiyo kufikisha jumla ya poiinti 35 ikiwa nafasi ya pili.


Akizungumza na Saleh Jembe, Habib Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC amesema:" Kuhusu maamuzi ndani ya uwanja hilo benchi la ufundi hatujui, sisi kazi yetu ni kufundisha timu ili ipate matokeo na ndicho ambacho tunakifanya wakati wote.


"Ninachokijua mimi ni kwamba wachezaji wetu walipambana katika kusaka matokeo na tumepoteza hakuna cha kubadilisha zaidi ya mipango kwenye mechi zetu zijazo,".


Tukio hilo  lilichukua dakika nne kwa wachezaji wa KMC kuwa kwenye ubishani na mwamuzi kwa kuwa hawakukubaliana na kitendo hicho .

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad