Wabakaji Pakistan kuhasiwa kwa kemikali




Maandamano dhidi ya ubakaji yamekuwa yakifanyika kote nchini Pakistan katika miezi ya hivi karibuni baada ya ubakai mbaya uliotokea mwezi Septemba.
Rais wa Pakistan amesaini sheria mpya itakayotoa adhabu kali dhidi ya wahusika wa ubakaji.

Kulingana na sheria hii , serikali itaweka sajiri ya watu wanaopatikana na makosa ya ubakaji, kulinda utambulisho wa waathiriwa na matumizi ya kemikali kuwahasi baadhi ya wabakaji.

Kulingana na sheria hii, kesi za ubakaji zitaharakishwa. Mahakama zinatarajiwa kukamilisha kesi ya ubakaji ndani ya kipindi cha miezi minne.

Serikali imesaini sheria mpya dhidi ya ubakaji baada ya malalamiko megi ya watu dhidi ya unyanyasaji huo wa kingoni baada ya wanaume kadhaa kumbaka mwanamke mmoja nje ya jiji la Lahore.

Walimbaka mwanamke huyo kando ya barabara inayoelekea katika jiji hilo mbele ya watoto wake wawili. Mkuu wa polisi alisema kuwa muathiriwa kwa upande mmoja alikuwa na makosa.

Kauli yake pamoja na unyanyasaji huo wa kinyama viliwakasirisha watu nchini humo ambao walisema kuwa amegeuza ukatili huo kuwa kitu kidogo. Maandamano makubwa yamekuwa yakiendelea kuilazimisha serikali kuchukua hatua dhidi ya ubakaji.

Waziri Mkuu Imran Khan na baraza lake la mawaziri waliidhinisha sheria hiyo na Rais Arif Alvi akaisain kuwa sheria Jumanne

Serikali ilipewa siku 120 na umma kuwa imeidhinisha sheria hiyo na kupitishwa na bunge.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad