Uongozi wa klabu ya Simba SC kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wake Barbara Gonzalez amethibitisha kuwatoa baadhi ya wachezaji kwa mkopo ili kukuza uwezo wao, baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao watetezi wa VPL.
Wachezaji ambao huenda wakatolewa kwa mkopo ni kiungo Ibrahim Ajibu, mshambuliaji Miraji Athumani, mlinzi Kennedy Wilson Juma, Ibrahim Ame na mshambuliaji Charles Ilanfya ambao wawili hao huu ni msimu wao wa kwanza klabuni hapo.
Washambuliaji Miraji Athumani, Charles Ilanya na mlinzi Ibrahim Ame wanahusishwa kwenda kukipiga kwenye klabu ya Ihefu ya jijini Mbeya, ikiwa ndiyo klabu pekee inayoripotiwa kuuandikia uongozi wa Simba kuomba uwezekano wa kuwatumia wachezaji hao kwa mkopo.
Klabu ya Ihefu ambayo ni ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa VPL imedhamiria kubaki ligi kuu msimu huu, kwani tayari wamewasajili kipa Deogratius Munisi, washambuliaji Juma Mahadhi kutoka Yanga na kiungo Joseph Mahundi na Andrew Simchimba kutoka Azam FC.
Kiungo Ibrahim Ajib yaelezwa kumendewa kwa muda mrefu na wauaji wa kusini, klabu ya Namungo ili asaidiane na kiungo wake Luca Kikoti 'Mtakatifu wa Kusini', kutengeneza nafasi zaidi za mabao klabuni hapo.