Wafahamu Mabilionea 5 Walioongeza Utajiri Wao zaidi 2020

 


Tayari walikuwa mabilionea ... lakini utajiri wao uliongezeka zaidi mwaka 2020.

Bila sha mwaka huu unaoelekea kumalizika ukilikumbwa na changamoto nyingi kwa watu wengi, huku zaidi ya watu milioni 1.6 wakifariki kutoka na janga la covid-19 kote duniani na mzozo wa kiuchumi uliosababisha biashara nyingi kufungwa na mamilioni ya ajira kupotezwa.

Hata hivyo watu tajiri zaidi duniani hawakuathiriwa na janga hilo.

Zaidi ya asilimia 60% ya mabilionea duniani waliongezea utajiri wao mwaka 2020 na watano wa kwanza ambao waliongezea utajiri wao kwa pamoja walikuza mali yao kwa dola bilioni 310.5.

1. Elon Musk, Mwanzilishi mwenza na Afisa mkuu mtendaji wa Tesla

Elon Musk, mwanzilishi wa kampuni ua SpaceX na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tesla, ameongeza takriban dola bilioni 140 ya biashara yake ya mwaka 2020

Kutokana na hilo utajiri wake uliongezeka wa dola milioni 167,000 Jumatatu, kwa mujibu data kutoka Bloomberg .

Hii ilitosha kumfanya Musk kupanda nafasi kadhaa katika orodha ya mabilionea na kumpita Bill Gates kuchukua nafasi ya pili (baada ya Jeff Bezos) mwezi Novemba.

Pia kulingana na jarida la Forbes ,hii ni mara ya kwanza katika mwaka bilionea kuongeza utajiri wake kwa kiwango hicho tangu jarida hilo lilipoanza kufuatilia mali ya ya mabilionea dunian.

2. Jeff Bezos, mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Amazon

Jeff Bezos, ambaye pia ni mmiliki wa gazeti la Marekani la The Washington Post , alianza mwaka 2020 kama mtu tajiri zaidi duniani na kuumaliza akiwa vivyo hivyo.

Alichofanya ni kuongeza zaidi ya dola 72 katika thamani yake, iliyochangiwa na ongezeko la mauzo ya mtandaoni katika kampuni yake Amazon kutokana na janga la corona.

apo hana mazoea ya kufanya shughuli za kutoa misaada, mwaka huu alijaribu kufanya hivyo: mwezi in Februari alitoa msaada wa dola bilioni 10 kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na mwezi Novemba alitoa karibu dola milioni 800 kusaidia mashirika ya mazingira.

Mtalaka wake Mackenzie Scott alitoa msaada wa karibu dola bilioni 5.8 kwa mashirika ya kutoa misaada mwaka.

Mackenzie Scott, ni mmoja wa wanawake tajiri duniani, hutoa karibu dola bilioni 6 kutoka kwa utajiri wake.

3. Zhong Shanshan, mwanzilishi wa kampuni ya Nongfu Spring

Thamani ya utajiri wa Zhong Shanshan iliongezeka hadi $ 62.6 billion (kwa sasa ni zaidi ya $ 69 bilioni), kwa mujibu wa Bloomberg.

Zhong alikuwa mtu tajiri zaidi wa China mwezi Septemba baada ya kampuni yake ya maji ya chupa, Nongfu Spring, kufanikiwa katika uuzaji wa hisa zake kwa umma na kupata dola bilioni 1.1 za Marekani.

Kampuni hiyo aliyoanzisha mwaka 1996 inadhibiti and controls a fifth of the bottled water market in the Asian giant has a value of about US $ 70,000 million.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 66-pia anamiliki karibu asilimia 84 ya kampuni hiyo, utajiri unaokaridiwa kuwa karibu dola bilioni 60.

Hii ilimsaidia kuwapiku mabilionea wengine kama vile mwanzilishi wa Tencent Pony Ma na Alibaba, Jack Ma kuwa mtu tajiri zaidi chini China katika miezi ya hivi karibuni.

Zhong pia anasimamia kampuni ya utengenezaji chanjo ya Beijing Wantai Biological Pharmacy, ambayo iliuzwa kwa umma mwezi Aprili.

Kampuni hiyo ilitengeza chanjo ya Covid- 19 ya kupuliza puani ambayo ilikuwa katika awamu ya pili ya majaribu mwezi Novemba.

4. Bernard Arnault, mmiliki wa maduka ya LVMH

Frenchman Bernard Arnault ndiye mtu tajiri zaidi katika nchi yake baada ya jarida la Forbes kumweka wa pil`i katika orodha ya watu tajiri zaidi, japo Bloomberg ilimuorothesha nambari 4.

Mmiliki wa kampuni ya bidhaa za kifahari za LVMH, Arnault anakamilisha mwaka huu akiwa na utajiri wa thamani karibu dola 146.3 bilioni.

Hata wakati ulimwengu ulikuwa unakabiliwa na janga la corona utajiri wa Arnault uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 mwaka 2020.

Janga la corona lilipotokea LVMH iliacha kwa muda mpango wa kununua Tiffany & Co., lakini mwezi Oktaba ilifikia mkataba wa kuinunua kwa karibu dola 15.8 bilioni, karibu dola za Marekani 400 milioni chini ya bei ya awali.

Uuzaji wa bidhaa za kifahari uliendelea kupungua, lakini LVMH iliwashangaza wawekezaji hivi karibuni ilipotangaza kuwa uuzaji wamikoba ya Louis Vuitton na Dior ulisalia imara, hususan katika nchi kama Korea Kusini na China.

5. Dan Gilbert, Rais wa kampuni za Rocket

Akiwa na umri wa miaka 58, Gilbert anamiliki timu ya mpira ya NBA Cleveland Cavaliers na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya uuzaji nyumba kwa mkopo ya Quicken.

Kwa mujibu wa data ya Bloomberg, thamani yake iliongezeka kwa dola 28.1 bilioni mwaka 2020 ( na kufikia $ 35.3 ), kutokana na kasi ya ukuaji ya kampuni mzazi ya Quicken Loans, Makampuni za Rocket, uzinduzi wa toleo la Umma mnamo Agosti.

Gilbert anamiliki 80% ya kampuni za Rocket, ambayo thamani yake inakadiriwa kuwa zaidi ya dola 31 billioni.

Utajiri wa Gilbert uliongezeka mwaka 2020 (mara sita zaidi kwa mwaka) kutokana na na uuzaji wa hisa za Quicken kwa umma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad