Watu 21 wauawa kwenye shambulio la kujitoa muhanga nchini Somalia



Idadi ya watu waliouawa kwenye shambulio la bomu katika mji wa Galkayo nchini Somalia imeongezeka na kufikia watu 21. 
Kundi la kigaidi la Al Shabaab limedai kuhusika na mashambulio hayo. Msemaji wa serikali ya jimbo la Gamudung amesema wengi waliouawa ni wanajeshi wakiwemo makamanda watatu wa kijeshi baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujilipua. 

Watu wengine 19 walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Waziri Mkuu wa Somalia Hussein Roble alihudhuria mazishi ya wanajeshi waliouawa kwenye mlipuko huo na amelaani tukio hilo ambalo aliliita la kigaidi. 

Mlipuko huoulitokea karibu na uwanja wa michezo siku ya Ijumaa ambapo watu walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya kumkaribisha waziri mkuu Roble. Kundi la Al shabaab limesema mlengwa hasa alikuwa ni waziri Mkuu huyo wa Somalia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad