Wema Sepetu "Nakiona Kifo Changu, Afunguka Mazito"



PISI kali kwenye Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu amesema kuwa, ameumwa kiasi cha kuona dalili zote za kifo chake, IJUMAA WIKIENDA lina habari kamili.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Wema anasema akipona kabisa atasoma dua ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumkirimia wema wake.


Akifafanua zaidi, Wema anasema anasumbuliwa na homa ya mapafu (pneumonia), ambayo ilikuwa ikimfanya ashindwe kupumua kwa kumbana kifua.“Yaani naona ndiyo mwisho wangu duniani ndiyo maana nilituma picha kwenye Mtandao wa Instagram ili watu wakisikia lolote wajue kuwa nilikuwa ninaumwa.

NASHINDWA KUPUMUA


“Watu wanaweza kuhisi utani, lakini nataka niwaambie ukweli kwamba kwa namna nilivyokuwa ninaumwa niliona wazi kifo kipo karibu yangu kabisa kwa sababu nilikuwa nashindwa hata kupumua na nikaona naweza kufa bahati mbaya watu wakajua labda ninafanya utani… lakini kweli niliumwa sana,” anasema Wema.Staa huyo anaongeza kuwa anamshukuru sana Mwenyezi Mungu anaendelea kupumua vizuri tofauti na mwanzo


Pia Wema anawasisitiza mashabiki wake waendelee kumuombea bila kuchoka maana tatizo lake linaisha na kujirudia.“Mashabiki wangu waendelee kuniombea maana tatizo langu linakuja na kuondoka, lakini angalau kwa sasa ninaendelea vizuri tofauti na mwanzo ilivyokuwa,” anasema Wema.


HOMA YA MAPAFU NI NINI?


Kwa mujibu wa Dk Sadick Sizya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar, homa ya mapafu au pneumonia ni ugonjwa unaoathiri na kuua mamilioni ya watu kila mwaka duniani. Anasema ugonjwa huo ni mojawapo ya sababu kumi za vifo vinavyotokea kwa watu wazima.“

Pneumonia ni maambukizi katika viriba vya hewa katika pafu moja au mapafu yote. Viriba hivi vya hewa huweza kujaa maji au usaha na kusababisha mgonjwa kukohoa, homa kali na kupumua kwa shida. Pneumonia hubebwa na bakteria, virusi au fangasi,” anasema.Anasema Pneumonia inaweza kuwa ya kawaida na ikapona, lakini wakati mwingine huwa ni tishio kwa uhai na huweza kusababisha kifo.

“Ugonjwa huu mara nyingi huwapata watoto wadogo au watu wenye umri zaidi ya miaka 65, lakini pia huweza kuwapata watu ambao mfumo wao wa kinga mwilini umeshambuliwa na magonjwa nyemelezi,” anasema.

DALILI ZA UGONJWAA

nasema kuwa, dalili za ugonjwa huo ziko za aina mbalimbali na hutofautiana kutoka dalili za awali hadi zile ambazo ni kubwa zaidi.

“Tofauti ya dalili wakati mwingine haisababishwi na muda tu ambao mgonjwa ameugua, bali pia ni nini kimesababisha, umri wa mgonjwa na kinga yake ya mwili kwa jumla. “Dalili za kati, kawaida huwa kama za mafua au kikohozi, lakini hudumu kwa muda mrefu.“Dalili huweza kuwa; maumivu ya kifua unapokohoa au kuhema. Kuchanganyikiwa ambayo hutokea kwa watu ambao wana umri zaidi ya miaka 65.

Kikohozi kizito. Uchovu usioisha. Homa, kutoka jasho na kutetemeka mwili.“Dalili nyingine ni joto la mwili kushuka kuliko kawaida (hii pia hutokea kwa watu ambao wana umri zaidi ya miaka 65 au wana kinga pungufu ya mwili). Kichefuchefu, kutapika na kuharisha na kuishiwa pumzi.

HUSABABISHWA NA NINI?

Dk Sizya anasema kuwa, sababu kubwa ya homa ya mapafu huwa ni bakteria ambao wako katika hewa tunayovuta. “Kawaida kila siku unavuta bakteria hawa, lakini mwili unajilinda ili wasilete tatizo kwenye mapafu yako. Lakini wakati mwingine vimelea hivi huizidi nguvu kinga yako ya mwili, wakati mwingine hata kama afya yako ni nzuri,” anasema daktari huyo maarufu.

NJIA ZA KUJIKINGA NA PNEUMONIA

Aidha, anaongeza kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo, tunapaswa kuweka mazingira kwenye hali ya usafi ili kupunguza uwezekano wa kuchukua vimelea kutoka sehemu mbalimbali endapo mgonjwa wa pneumonia atagusa vifaa ambavyo mtu mwingine.

“Usitumie sigara kwani moshi wa sigara hupunguza uwezo wa mapafu kudhibiti vimelea vya pneumonia hivyo kufanya kuwepo uwezekano wa kuambukizwa pneumonia. Pia tunapaswa kupata chanjo ya pneumonia ili kujikinga na ugonjwa huu,” anasema.

AFYA YA WEMA

Afya ya Wema ambaye ni kinara wa Bongo Movies imekuwa ikiibua mjadala mzito hasa baada ya kupungua mwili kiasi cha kuibua hofu kwa miezi kadhaa iliyopita hadi sasa.Yapo madai kwamba, yeye mwenyewe ndiye aliyeamua kujikondesha makusudi baada ya kuchukizwa na umbo lake la ubonge.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad