Yanga Yatuma Salamu kwa Tanzania Prison "Tutawanyoa Vipara na Kisu"



 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Alhamisi, Uwanja wa Nelson Mandela.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa mzunguko wa pili msimu wa 2020/21 baada ya mzunguko wa kwanza kumeguka.


Yanga imefunga pazia la mzunguko wa kwanza ikiwa imekusanya jumla ya pointi 43 ipo nafasi ya kwanza na haijapoteza mchezo hata mmoja.


Itakutana na Tanzania Prisons, Desemba 31 ikiwa ni mchezo wao wa mwisho kwa mwaka 2020 kabla ya kuanza mwaka mpya 2021 kwa Neema ya Mungu.


Kaze amesema:"Wachezaji wapo vizuri na mazoezi ambayo wameyafanya ni mazuri yananipa picha kwamba tunakwenda kupata matokeo ugenini,".


Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ngoma ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, ilikuwa ni mechi ya kwanza na ya mwisho kwa Farouk Shikalo kukaa langoni kwa mzunguko wa kwanza

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad