"Nyumba zimejaa Popo, hovyo kabisa" - Waziri Mkuu



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameipa wiki mbili Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuhakikisha kwamba ifikapo Januari 1, 2021, Bandari ya kimkakati ya Kagunga iliyoko katika Kata ya Kagunga wilayani Kigoma iwe imeanza kutoa huduma.

Ametoa agizo hilo jana jioni, baada ya kukagua mradi wa bandari ya Kagunga iliyopo kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika, wilayani Kigoma, ambapo alichukizwa na kitendo cha bandari hiyo kushindwa kutoa huduma licha ya kuwa imekamilika.




"Leo nimekuja hapa kuona bandari, hii bandari ilikamilika mwaka 2017 imekaa tu, nyumba zimejaa popo tu na mle ndani kumejaa takataka na mmefagia jana baada ya kusikia mimi nakuja, hovyo kabisa nawauliza hapa wanajikanyaga tu, tuna mtumishi hapa, hakuna mtumishi amekuja jana badaa ya kusikia nakuja, hovyo kabisa hawa", amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema mbali na bandari hiyo ya Kagunga kuanza kazi Januari Mosi, 2021, pia ameagiza soko la kisasa la Kagunga nalo lianze kazi siku hiyohiyo ili kuwawezesha wananchi wa Kagunga waanze kufanya biashara na kuinua kipato chao

Pia, Waziri Mkuu alishangazwa na kuchukizwa na kitendo cha Meneja wa Bandari kutoka Makao Makuu ya TPA ambaye hajawahi kufika katika bandari hiyo na haijui, "Kama kweli wewe ni Meneja wa Bandari Tanzania, bandari zako huzijui na un amiaka chungu nzima unafanya kazi gani, hovyo kabisa".

Waziri Mkuu alisema mradi wa ujenzi wa bandari hiyo ulikamilika 2017 ukihusisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na la mizigo, nyumba ya kuishi mtumishi na jengo maalumu lakini hakuna mtumishi katika bandari hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu shilingi bilioni 3.8.

"Tarehe moja ya mwezi wa kwanza mwaka 2021, nataka bandari hii ianze kazi, nenda mkajipange, hapa hakuna mtumishi hamisha watumishi kama wapo Dar es Salaam, kama wapo Kigoma leta watumishi hapa wawatumikie wananchi kwenye bandari hii".

Aidha Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wa TPA waruhusu meli na boti za watu binafsi zifanyekazi ya kutoa huduma katika bandari hiyo ili kuwawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha mizigo kwa urahisi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante Kassim, Watendaji mjipange ki Sawasawa, Amkeni katika kuwajibika..!! Awamu ya Tano Muhula wa pilihakuna kupoteza wakati katika kumtumikia Mtanzania aliempaDeni kubwa la Imani kwa Jemedari wetu JPJM.

    Ukiangalia Baraza lake, NI UJUMBE TOSHA.

    UPIGAJI NA UZEMBE SASA BASI. TANZANIA MPYA INAKUJA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad