TIM ZOOK, mtaalam wa mashine za x-ray, kutoka Santa Ana, California, Marekani, aliyefurahia kuchanjwa dhidi ya virusi vya corona, alifariki siku kadhaa baadaye ambapo mkewe, Rochelle, alisema hilo lilitokana na chanjo hiyo ilivyofanya kazi hasi katika mwili wake.
Zook aliandika katika mtandao wa Facebook: “Nimefurahi sana kupata chanjo. Hivi sasa nimejikinga kikamilifu baada ya kupata dozi yangu ya pili ya Pfizer Januari 5.
Mtu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 60 alirusha picha ya mkono wake katika mtandao huo ikiwa na plasta sehemu aliyochanjwa pamoja na kadi ya kuonyesha kuchanjwa kwake. Lakini, saa kadhaa baadaye, Zook alianza kupata maumivu ya tumbo na kuanza kupata matatizo ya kupumua.
Wafanyakazi wenzake walimpeleka kwenye matibabu ya dharura hospitali ya South Coast Global Medical Center, ambako baada ya matibabu alifariki.
Mamilioni ya chanjo dhidi ya Covid-19 yametolewa nchini Marekani tangu Desemba 2020 ambapo ni watu wachache wameathirika na chanjo hiyo.
Marekani imerekodi matukio milioni 25.4 ya ugonjwa huo na vifo 425,250.