Aggrey Morris kuagwa rasmi mechi ya Taifa Stars

 


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, limetangaza mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, utatumika kumuaga mchezaji Aggrey Morris ambaye ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa.


Agrrey Morris  alianza kuitumikia Taifa stars mwaka 2010 na takwimu zinaonyesha amecheza jumla ya michezo 35 akiwa amefunga mabao 2 kwenye michezo hiyo, na mchezo wa Januari 10 dhidi ya Kongo ndio utakuwa mchezo wake wa mwisho baada ya miaka takribani 10 ya kuitumikia Taifa stars.


Taaarifa iliyotolewa na shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF imesema, “Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa Taifa Stars vs DR Congo, Januari 10, 2021 utakaochezwa uwanja wa Mkapa, utatumika kumuaga Aggrey Morris, baada ya kulitumikia Taifa na kutangaza kustaafu kucheza Taifa Stars”.


Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha cha Taifa stars kuelekea kwenye fainali za michuano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN), ambayo itafanyika nchini Cameroon, kuanzia Januari 16, Taifa Stars watacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Kongo, mchezo wa kwanza utachezwa Januari 10, 2021 na wapili utachezwa Januari 13, 2020. Michezo yote hii itachezwa uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.


Aggrey mwenye umri wa miaka 36, bado anakipiga kwa upande wa klabu yake ya Azam FC na ndio nahodha wa kikosi hicho, alijiunga na wauza Ice Cream hao mwaka 2009 akitokea Mafunzo ya visiwani Zanzibar.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad