BENCHI la ufundi la AS Vita, limeweka wazi kuwa wamefurahia kupangwa tena na Simba katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili walipe kisasi cha kutolewa na Wekundu hao msimu wa 2018-19.
Simba imepangwa kundi A ikiwa na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita kutoka DR Congo na El Merrikh ya Sudan.
Simba ina kumbukumbu ya kukutana na AS Vita na Al Ahly katika msimu wa 2018-19 baada ya kupangwa kwenye kundi moja, ikawatoa nishai AS Vita kwa kuwafunga 2-1 jijini Dar na kuwatupa nje huku wao wakisonga mbele pamoja na Al Ahly.
Akizungumza na Championi Jumatatumoja kwa moja kutoka Kinshasa, DR Congo, Kocha Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu, alisema hawatakubali kufanya makosa waliyofanya msimu mmoja uliopita mbele ya Simba kwa kuwa wanataka kufika mbali kwenye michuano hiyo.“
Kwanza kwetu limekuwa jambo la furaha kupangwa tena na Simba kwa sababu sasa hivi tunawajua vizuri wakiwa nyumbani kwao wanakuwaje na hata wakitoka nje ya kwao lakini hawataweza kutoka safari hii katika mikono yetu. Safari hii wataona tutakavyowafanya kwenye mechi zote,” alisema Shungu